MPENZI WAKO NDIYE ADUI YAKO
IMEANDIKWA NA
CHIWAMBO, A. R. (2011)
MAPENZI
Kila
binadamu hupenda jambo fulani. Mapenzi ya mtu juu ya jambo yaweza kumvutia
kiasi kwamba anaweza kupoteza welekeo wa maisha yake. Watu hupenda hadi
kileleni. Hapa ndipo mtu aelewi hili wala lile. Hali hii si tu kwa vijana
wanaoingia katika umri wa balehe bali hata kwa wale waliovuka umri huu. Kweli
kila mtu anahaki ya kupenda. Na mapenzi haya yalianza pale binadamu walipoanza
kuishi pamoja kama mke na mume kama vitabu vyetu vya dini vinavyoelekeza,
ambavyo ni Biblia na Kuruhani.
Napenda
kuwa muwazi sana juu ya aina ya penzi ninalozungumzia. Ni yale mahusiano ya
kimwili yaliyopo kati mwanamke na mwanaume. Haya ndiyo mahusiano
ninayozungumzia na sizungumzii yale ya watu wa jinsia moja. Mapenzi hayauzwi na
ayachagui rangi wala kabila.Mapenzi ni kitu asilia ambacho humkuta mtu juu ya mtu mwingine ambaye
anaweza kuwa mwanamke kwa mwanaume au kinyume chake. Na hawa kila mmoja hutokea
kumpenda mwenzake mpaka kufikia kilele cha penzi.
Angalia
mfano huu; umepita wapi na kutembea mikoa mbalimbali au wilaya, tarafa, kata,
vijiji na mitaa mingapi? Umekutana na wangapi wazuri (wanawake au wanaume), na
ulimpenda yupi. Inawezekana kati ya uliowachagua hakuna hata mmoja kati ya wale
uliokutana nao ukaridhia kuwa naye. Lakini ulikutana na kijana mmoja ambaye
amekuvutia sana zaidi ya asana na mahusiano ukaanza kuanzisha mpaka leo ni mke
wako au mchumba wako. Hapo ndipo ninaposema “love is something natural”
na si kitu cha kubahatisha tu.
Na ieleweke kwamba mke mzuri ni wako
tu, na mme mzuri ni wako tu.
Hakuna ubishi kwa hili. Na pale unapoona kuwa mke au mme wako si mzuri basi
ulikosea wakati wa uchaguzi wako. Hapo huna
budi kuonyesha unampenda kama kitabu hiki kinavyoeleza uk.6 & 7. Na ujue
kwamba kila mtu ana haki ya kupendwa na mme, mke au mchumba wake. Penye upendo pana mapenzi ya kweli.
NINI MAANA YA MAPENZI?
Neno
mapenzi ni pana sana. Na kila mtu
huweza kufikiri kulingana na uelewa wake juu ya mapenzi kati ya mtu na mtu.
Mapenzi ni ile hali asilia ambayo mtu anakuwanayo kwa mtu mwingine na inapaswa
kuwa na makubaliano baina ya wahusika ambayo yaweza kuwa ya muda mfupi au muda
mrefu. Wengine husema mapenzi ni ile hali ya mtu kuwa na mahusiano ya kimwili na mwingine.
Kipindi
tulichopo sasa ni kipindi cha utandawazi.
Si mtoto mdogo si wakubwa wote wanayafahamu mapenzi yalivyo. Kwa sasa imekuwa
kawaida kwa kila mtu kuanza uhusiano hata kabla ya kufunga ndoa. Hii ndiyo
ninayoita utandawazi. Watoto wadogo hupata habari hizi kupitia masimulizi
kutoka kwa kaka na dada zao nyumbani au nje. Hii haikuwa tamaduni yetu, lakini
sasa ni jambo la kawaida kwa mwanafunzi wa darasa la tano kukutwa na ujauzito.
Lakini ni kwa mazingira hayahaya.
Kipindi
hiki ndicho kipindi kigumu kwa vijana kujua yupi ni mke/mme mwema na yupi si
mke/mme mwema. Athari hizi huwakuta sana akina dada ambao wakizidisha miaka
ishirini na saba, yule ambaye alikuwa mme mzuri anampoteza ndani ya miaka 18 hadi
miaka ishirini. Ndani ya miaka hii mwanamke huvutia na anaonekana kama ua
linalovutia wadudu (Dr Isack Ndodi, 2011). Nakubaliana sana na maneno ya Dr.
Ndodi akizunguma Channel 5 kati ya
mwezi Mai hadi Juni, 2011.
Kuna
ukweli uliopo juu ya hili. Ndani ya miaka hii mwanamke ujikuta anaingia katika
majaribu yasiyo na msingi huku akijitahidi kutafuta mme mzuri kwake, na matokeo
yake huishia kuchezewa na hatimae kukosa wote. Wanaume ndio wasababishaji
wakubwa wa mke huyu asiolewe au asipendwe. Angalia mfano huu, mti ukichipuza
maua utamuona mdudu wa kila aina akiwemo nyuki, nzi, kipepeo na wengine wemgi
wakiingia na kutoka. Haya ndiyo yaliyopo kwa wanawake kwa kipindi hicho tajwa
hapo juu.
Hapa
lile neno langu love is something natural (mapenzi ni kitu cha asili) hutumiwa
vibaya na badala yake mapenzi hupoteza umaana wake. Kwa kila mtu mwenye upendo
wa kweli hawezi kumdarau mchumba au mke/mme wake. Na inapotokea vinginevyo ni
makosa ya kibinadamu ambayo hutokea baina ya hawa wapendanao.
NINI MAANA KUPENDA AU KUPENDWA
Inawezekana
si mara yako ya kwanza kusikia nini kupenda. Haya yamewai kuzungumzwa na msanii
wa muziki Mwijuma Mumini. Neno kupenda lipo katika nyoyo za binadamu na uwezi
kuona kwa macho. Kwa kifupi ni neno la kufikirika tu. Lakini utagundua kweli
unapendwa na kupenda mara baada ya kukutana na mke, mme au mchumba wako.
Matendo ndiyo yanayoonyesha kweli unapendwa au unampenda.
Kwa
kawaida mtu anayetaka kuwa na mahusiano na wewe
huanza kuonyesha kwa sura pamoja na maneno yaliyojaa utamu. Na mara
uyasikiapo maneno hayo ndipo hamu na shauku ya kuendelea kuwa naye inakujia na
hatimaye mwisho wa siku mnaamua kuwa na makubaliano. Kwa kuwa utamaduni wa
baadhi ya jamii katika bara letu la Afrika unamnyima mwanamke kutamka neno
nakupenda kwa mwanaume, basi hapo lugha itayotumika ni ile ya ishara ya kuweza
kumvutia mwanaume kwa kila hali ili awe naye katika ukrasa wa mapenzi.
Na
pale mwanamke anapotamka neno nakupenda “I love you” kwa mwanaume, inaonekana
mwanamke yule ni mmalaya wa hali ya juu. Hii ni tofauti na nchi za Magharibi
ikiwemo marekani ambako mwanamke au mwanaume ana uwezo wa kuomba uhusiano wa
kimapenzi. Kwa Tanzania kulikuwa na neno “USIONE
SOO SEMA NAE”. Hili neno lilikuwa zuri kuwapa utambuzi wanawake wa kiafrika
kuweza kuomba uhusiano wa kimapenzi kwa mwanaume ampendaye na si kutegemea
afuatwe.
Tabasamu
zito, na tabia ya mwanamke huanza kuonyesha kuwa ni bora au mzuri kuliko za
wengine. Lingine ni kwamba maneno ya kumsifu mtarajiwa yanakuwa mengi. Mara
umependeza, mara leo tutoke out (kwenda kupumzika eneo fulani kama vile maeneo
ya starehe au sehemu yeyote waipendayo watarajiwa). Na hapo ndipo mmoja kati
yao huanza kutamka neno linalostahili ili kuwezesha mahusiano, na kuna wengine
hufikia kutamka hata kama ni siku ya kwanza kuonana/kukutana. Haya ni baadhi tu
ya mambo yanaoonyesha kuwa mtu anapenda au anapendwa kabla ya kuanza mapenzi
motomoto.
MWANZO WA MAPENZI
Mapenzi
huanza na moto wa hali ya juu. Kila mmoja anataka na kupenda kukaa wote muda
wote. Kila neno linalozungumzwa na mmoja wao huonekana zuri. Hapo ndipo mke au
mwanaume huamua kutoloka kwao na kumfuata mwenzi wake. Hapa wapendanao hujikuta
kama wapo nchi nyingine. Maneno ya utamu kama neno nakupenda hutamkwa kwa sana
tena kwa mkazo kwa wakati wote.
Kila
mmoja huona amefika sana. Na mara nyingi mtu awezi kuamini jambo lolote
analoambiwa na mtu mwingine. Haya yameonekana sana katika Tamthilia
zinazopendwa na vijana wengi kama zile za nchi za Magharibi. Mfano ni ile
iliyogusa nyoyo za watu wengi maalufu kwa jina la “Malichui” au AN ENGEL. Na LOVE TO DEATH.
Penzi
hufikia kileleni na wengine huanza hatua za utambulisho kwa wazazi. Kwa sasa
utambulisho huu hufanya na mototo mwenyewe. Hii ni tofauti na miaka ile ya
nyuma ambapo mme au mke huchaguliwa mke au mme na wazazi wake. Haya ndiyo mambo
ya sasa. Kila kitu uwekwa wazi na wapendanao wenyewe.
Kwa
wale wanaobahatika kuweza kufunga harusi uweza kufunga harusi na wangine
huishia njiani bila mafanikio kutokana na sababu mbalimbali zilizo nje au ndani
ya uwezo wao. Sababu ni nyingi hivyo mwandishi hakuweza kuzitaja zote lakini uk
7 & 8 zinajieleza wazi.
KUTENDWA
Hili
ni neno lililoibukia siku za hivi karibuni na kuonekana kuwa ni umaarufu sana
miongoni mwa vijana. Watu hutumia neno hili wakimaanisha kuachwa na mwenza au
mpenzi pasipo kutarajia kutokana na matendo aliyofanyiwa. Hii ndiyo tafsiri
yake. Ni mara nyingi sana jambo kama hili limewatokea wapendanao. Wangine
husema amemwagwa au amebwagwa chini. Hii ni misemo ya vijana wetu wa siku hizi.
Inawezekana kwa wengi na si wewe tu umewai kusikia neno hili la kutendwa. Si
geni kiasi kwamba mtu anaweza kutoelewa kinachoozungumzwa.
MAMBO MAKUU YANAYOSABABISHA
KUTENGANA KWA WAPENDANAO
1. Kutofanya
uchaguzi ulio sahii wa mke/mme au mchumba. Vijana wengi siku hizi hujilaumu sana juu ya chaguo la
mwenza wake. Ukikosea mwanzo ujue utaoa na kuacha mke zaidi ya mmoja. Pakifikia
mahali unaanza kutamani wanawake/mwanaume wa nje na kumsahau wako wa ndani ujue
ni ishara kwamba hukufanya chaguo zuri ujana wako.
2. Wazazi
kutopendezwa na mke/mme.
Hapa wazazi nawazungumzia wale wanaopenda kuingilia mambo ya ndani ya watoto
wao. Kuna watu wanaitwa mawifi, hawa ndio chokochoko kubwa na mke na mme
kutengana. Watatumia maneno ya uzushi na unafiki ili mradi mke au mme yule
waachane. Mwisho ndoa au uchumba unavunjika.
3. Dini
tofauti. Hili ni
suala la mdahalo karibu dunia mzima. Inapotokea mme na mke wameanzisha uchumba,
na kila mtu ana dini yake, mwanzo wa penzi hakuna aneyekumbuka nini athali kwa
hapo baadaye. Muda unasonga, na kila mmoja anahitaji afunge ndoa au wazazi
wafahamu, hapa kila mmoja anaanza kukumbuka utofauti wao. Kutokana na imani
kali au kutokuwa na uelewa mwanzo, wanaamua kutengana ili kulinda maslahi ya
dini au dhehebu la kila mtu. Hii mara nyingi hutokea kama mmoja wao ni Mkristo
au Muislam. Katika ndani ya ukristo kuna misingi inayoongoza kanisa la SABATO.
Hapa pia hawaruhusu muumini kuoa au kuolewa nje ya dhehebu hili vinginevyo anatengwa na kanisa.
4. kutofikia
kilele wakati wa tendo la ndoa. Hakuna ndoa inayoweza kudumu kama tendo la ndoa halifanyiki.
Au kama linafanyika ni kwa kulidhika mmoja na mwingine asitosheke. Hii ni
sahemu muhimu sana inayomfanya mke au mme aweze kuwa na mahusino na mtu
mwingine ili aweze kujitosheleza. Kila mmoja hupenda atosheke, na inapotokea
vinginevyo migogoro huanzia hapo na hatimae kuvunjika kwa penzi lao. Zao la
hili ni kutoroka kwa mke/mme au mchumba na kuanzisha uhusiano na mtu mwingine.
5. Tabia
ya uzinzi kupindukia.
Hapa nazungumzia tabia ya umalaya ya mwanamke au mwanaume nje ya mpenzi wake.
Hawa ni watu ambao uzaliwa na genes za aina hiyo na wamerithi kutooka kwa
wazazi. Hivyo kwa mtu aliyorithi inakuwa ni rahisi zaidi kutoka nje ya ndoa
yake na kwenda kufuata wengine ili mradi atimize malengo yake. NB. Tumetoa njia
za kutatua hili katika kitabu hiki.
6. Maneno
au mawasiliano.
Namna mke na mme wanavyozidisha mawasiliano, ndivyo wanovyoongeza penzi lao.
Kwa zamani barua zilikuwa ndio chombo cha mawasiliano kama mmoja wao aliishi
mbali. Lakini kwa sasa ni njia ya simu za mkononi. Inapotekea mawasiliano
yanapungua kati ya mme na mke kinachofuata ni kusauliana. Kila mmoja atapata
wazo la kuwa na mwingine na hatimaye kuanzisha mahusiano mapya na yule ambaye
hakupenda kuwa naye. Usipokuwa makini juu ya hili lazima mutatengana tu.
7. Wivu. Hakuna penzi linaloweza kudumu kama
hakuna wivu. Na wivu huo uwe wa kiasi ambacho akiwezi kuathili penzi lao. Kuna
watu wana wivu kupindikia. Hili ni tatizo kubwa, na hakuna mtu anayependa
afanyiwe wivu kiasi kwamba hadi mtu anakosa uhuru. Pakifikia mahali hapa wapendanao
huanza kutoa maneno ya siri kwa jirani na mwishowe kutengana kwa wependanao.
Hapa pia inaambatana na hali ya kutokuwa na imani na mwenza wako.
8. Kuwa
na mahusiano ya hali ya juu na mtu wa jinsia tofauti pamoja na utani. Mtu ukishaolewa, kuoa au kuwa
mchumba ni bora zaidi upunguze mahusiaona ya kupindukia na watu wa jinsia
nyingine. Hali ya utani unaoambatana na kushikana, kubusiana pamoja na
kuelezana maneno ya kimapenzi kwa wale ambao si wapenzi wako husababisha
mgogoro na mwenza wako. Vinginevyo ndoa au uchumba ule utaelekea mahali pabaya
na mwisho kuvunjika kwa penzi.
9. Kusikiliza
maneno ya watu.
Kuna watu hupenda kuchonganisha wanawake au wanaume wa watu kwa maslai binafsi.
Kwa kawaida watu hawa wapo kwa ajili ya kuona mnagombana. Hivyo basi,
kusikiliza kwa maneno ya hawa watu inapelekea kubadili kwa mwenendo wa mweza na
hatimaye kuwa mwisho wa penzi.
10.
Ugumba/tasa. Hii ni ile hali ya mmoja kati ya
wapendanao kutokuwa na uwezo wa kuzaa. Yaani kwa mwanaume kushindwa kutoa mbegu
zinazoweza kusababisha kutungwa kwa mamba, na kwa mwanamke kushindwa pia kutoa
mayai yenye uwezo wa kupokea mamba. Hali hii huwaathiri sana wanawake ambapo
mke huonekana mzigo mzito katika nyumba. Wangine wanafikia mahali wanawaambia
wapenzi wao kuwa wanajaza choo tu. Hii kauli lazima ipigwe vita sana. Madhara
ya kauli zinazofanana na hizo, yule mwenye kizazi huamua kumwacha yule asiye na
kizazi na kwenda kufungua kizazi kipya na mtu mwingine.
Hizo ni baadhi ya sababu za kimsingi
zinazochangia uvunjifu wa ndoa au uchumba. Ukweli ni kwamba sababu zipo nyingi
lakini zinazoumiza sana vichwa vya watu ni hizi.Hivyo kila mtu anapaswa kuwa
makini juu ya mambo haya yaletayo mzozo katika penzi husika.
NAMNA YA KUTATUA NA KUEPUKANA NA
MAMBO YAWEZAYO KUSABABISHA KUTENGANA
Kufanya uchaguzi sahihi wa mchumba. Kila mtu anashauriwa kuchagua
mchumba anayekufaa. Si kila mwanamke au mwanaume ni mzuri kwako na kuanza
maisha kama wanandoa. Jaribu kutafakari na kupata ushauri wa watu walio karibu
naye ili upate juu ya tabia aliyonayo. Ukiona ni mzuri unaweza kuanza hatua za
kufunga harusi.
Si
vizuri kuparamia mwanaume au mwanamke unayekutana kwenye basi au kwenye
mitandao ya kijamii kama facebook. Kweli watu wanamaneno matamu na mazuri sana,
lakini walio wengi ni wababaishaji wa mapenzi. Jiulize swali dogo tu, ameonana
na wanaume au wanawake kama wewe wangapi. Jibu ni wengi, hivyo kuwa mtulivu,
siku ikiwadia utampata mzuri zaidi ya huyo (simahanishi mtengane na mme/mke au
mchumba uliyenaye sasa).
Wazazi hawana budi kupewa elimu ya
kutosha juu ya mke/mme au mchumba wako. Mwenye haki ya kuchagua mchumba ni wewe na sio wazazi
wako. Wewe ndiye unayefahamu unampenda kiasi gani. Jaribu kuwashauri hadi
wakuelewe kwa nini unataka kuwa na huyo mchumba wako. Hapa hauna budi kupunguza
hasira kwani wazazi wengine wana tabia ile ya kuhukumu mtu mara tu baada ya
kuanza kuongea naye.
Kama
wapendanao hamna budi kuendelea kushirikiana nao kwa karibu, na mwisho wa siku
hali waliyonayo itatoweka na badala yake uhusiano wenu utaendelea kukua.
Usiwatamkie maneno makali wale wote wanaokupinga juu huyo mchumba wako. Kwa
kufanya hivyo uhusiano wenu utadumu maisha milele.
Ni muhimu kuweka makubaliano juu ya
dini za wapendanao.
Hili ni jambo linaloumiza sana vichwa vya watu ulimwenguni. Suala hili ni suala
la mdahalo usio na mwisho, na uhishia tu pale wapendanao wanapoamua kufuata
majibu na mapatano yao.Kama mke/mme wako ni dini tofauti na yako, basi
nakushauri muanze kupanga mikakati pale tu mutapoamua kuanza uhusiano wenu.
Mweleze ukweli huyo mchumba wako juu ya dini yenu na mnavyoishi kule kwenu.
Baada ya hilo muendelee kupanga hatima ya kizazi chenu na athari zipi
zitawapata na mutatatua vipi hizo changamoto zote. Changamoto ambazo huathiri
sana ni hatima ya watoto. Hapa kama msimamo haupo juu ya maamuzi yenu basi
tambueni huo utakuwa mgogoro usio na mwisho. (Hapa nimezungumzia tu kwa wale
walio na wanaotarajia kuingia kwenye uchumba).
Kwa
wanandoa kama walifanya maamuzi bila kujijua basi nashauri waendelee kufuata
utaratibu wao na pale inaposhindikana muwaone wataalamu wa masuala ya mahusiano
katika jamii wakiwemo watu wa ustawi wa jamii.
Ni vizuri kumfikisha mwenza wako
kileleni. Wanaume
walio wengi hushindwa kuwafikisha wake zao kileleni. Hii yote inatokana na
kushindwa kujua namna gani ya kumwandaa mke au mchumba wake ili afikie
kileleni. Walio wengi wanaamini wakishafikia hatua ya kupezi mara mbili wanaona
wamemfikisha mke kileleni. Nakushauri usome kitabu kilichoandikwa na Dr Paul.
Mara nyingi husikika siku ya jumatano katika RFA (Radio Free Africa) kuanzia
saa tano usiku.
Utajua
namna ya kumfikisha mke wako au mme wako kileleni. Pia kuna wanaume ambao
hukosa kufikia kileleni. Hii husababishwa na mke kutojua namna ya kumfikisha
mme kileleni. Hivyo kupitia kitabu cha Dr Paul Nelson utaweza kujua sehemu zipi
zinapaswa kuguswa ili kumfikisha kileleni. Kitabu kinachozungumzia namna ya
kumfikisha mpenzi wako kinaandaliwa. Kwa wale wapenzi wa facebook munaweza
kutembelea ukrasa wangu wa facebook au Arasachi The Centre of Learning”
Kikiwa
tayari muda wowote utakiona sokoni. Kitakuja na kichwa cha habari kisemacho
“unafahamu namna ya kumwandaa mpenzi wako?”. Kulingana na mwili wa mwanamke
ulivyo, unaweza kufanya tendo la ndoa hata masaa mawili na asifikie kileleni.
Mke au mme akifanya vizuri juu ya hili hawezi kumtamani mme au mke mwingine kwa
sababu utakuwa umemjenga kisaikolojia.
Ni vizuri kujizuia tabia ya umalaya
kabla na baada ya kuanzisha uchumba. Hakuna mwenza anayependa kuona mke/mme wake anatabia ya
umalaya. Wengi huzaliwa nayo na kurithi kutoka kwa wazazi. Na wengine hujengwa
na makundi mchanganyiko katika jamii zikiwemo taasisi za kufundishia.
Kwa
mfano Vyuo vikuu nchini Kenya au nchi za Magharibi ni kawaida kuwaona wanafunzi
wakishikana sehemu mbalimbali za miili yao wakiwa maeneo tofauti tofauti ya
shule au chuo chao (hawa ni wanalika “peer group”).
Muhusika
hauna budi kujizuia kwa kuwa naye karibu yule mpenzi wako. Na inavyotokea
unaishi naye mbali basi mtembeleane wakati wa likizo na kupata muda wa kuongea
pamoja. Pia jiepushe kwenda maeneo ya starehe kama vile baa na ufukweni ukiwa
pekeyako pindi mpenzi wako yuko mbali nawe. Kwa kufanya hili tabia yako utakuwa umeizuia na kuiacha kabisa.
Mawasiliano lazima yadumishwe. Mwanzo wa penzi mawasiliano huwa ni
ya hali ya juu kwa sababu kila mmoja anapenda amjue vizuri mpenzi wake. Hii
yote hutokea kwa sababu ya upendo walionao kwa kila mmoja kwa mwenza wake. Siku
zinavyosonga mawasiliano huanza kufifia au kuongezeka kutegemeana na lugha
inayoyumika. Hali ya kufifia mara nyingu hutokea tu mara baada ya kuanza zoezi
zima la mapenzi kwa siku ya kwanza. Baadhi
ya wanaume hukosa hamu ya kuendelea kuwa naye kama mpenzi wake. Lakini baada ya
siku chache mkizidi kuwasiliana hali inarudi kama kawaida. Hii hutokea sana kwa
wanaume, na kama kwa wanawake ni kwa kiasi kidogo sana. Hapa ndipo utapoona
yule uliyempenda umetengana ghafla.
Mukifikia
hatua hii mnapaswa kuendeleza na mawasiliano. Kwani kitendo cha kutengana
ghafla huwaumiza sana wanawake kwa sababu inaonekana lengo kubwa ni kumchezea
na kumwacha. Ili kudhibiti hali hii mnatakiwa kudumisha mawasiliano na kuendelea
kuwa karibu sana na baada ya wiki moja hali itarudi na kuwa na hamu ya kuwa na
wewe muda wote. Hapo ujue kuwa hali imeshatoweka na sehemu iliyobaki ni ya
kuendelea kujipangia mikakati juu ya mahusiano yenu ili kudumisha penzi lenu.
(hali hii ni kwa baadhi tu ya watu na hutokea kama mke au mme hakuweza
kumfikisha kileleni mwenza wake. Ni vizuri mfanyie surprise ya ukweli siku ya
kwanza ili asikusahau kamwe maishani mwake. Walio wengi huikumbuka sana yale
yaliyotendeka siku ya kwanza kufungua penzi lao).
HATUA ZA KUJUA PENZI LINAPOTEZA UELEKEO.
Hatua kuu zinazoonyesha penzi
limepoteza uelekeo ni hizi hapa:-
1. MAWASILIANO KUWA DUNI
2. USO KUONESHA KUWA HAPENDI KUONGEA
3. HASIRA ZA MARA KWA MARA
4. MANENO YASIYOFAA HUANZA KUZUNGUMZWA
5. KUDAI KUTENGANA
1. MAWASILIANO KUWA DUNI
Mapenzi
na sawa na jani la mti. Huendelea kuwa na mawasiliano na shina kwa kusaidiana
na matawi. Ila siku ikifika jani linadondoka. Hii utokea pale jani linapochoka
na maisha ya kujishikiza. Haya ndiyo sawa yalio kwetu binadamu. Mwanzo uanza
kwa kasi zaidi na mwisho hufifia kwa mawasiliano. Mtu anaweza kukata
mawasiliano kwa sababu zake binafsi zikiwemo hizo za hapo juu.
Kama
mawasiliano yalikuwa ni mara tano kwa siku (kwa wale walio mbali, mfano
masomoni.), basi mawasiliano yanaaza kushuka hadi mara mbili hadi mwisho wa
siku mawasiliano kukaka kabisa. Hapa kila mmoja akiulizwa swali kwanini husema
nilibanwa na kazi ndio maana sikuweza kukutafuta.
Kwa
walio kwenye ndoa mawasiliano pia yanakuwa nyuma kidogo. Kama alikuwa
anakusalimia kwa kukumbatiana, hapa hali hua tofauti kabisa. Muda mwingine kila
mtu na kazi yake. Kila mtu shuka yake, na kukicha kila mtu kivyake.
Hii
hua na athari sana pale mmoja wa wapenzi anapokuwa na mpenzi mwingine. Yule
ambaye ulidhani umemchagua anakuja kuwa sumu kwako. Unapenda umwone yeye ataki.
Unapenda umpe zawadi yeye ataki, unapenda kutoka naye out yeye ataki, na pale
anaposema uwasiliane naye basi roho huweka pembeni. Utagundua kuwa kama
analazimishwa aongee.
Ikifikia
sehemu hii na kama ulimpenda kweli basi utaongeza jitihada za kutaka kuwa naye,
wasio na imani hufikia mahali wanasema nitaendelea kukaa bila kuoa. Kauli hii
ni udanganyifu tu. Akisahau yale yaliyomtokea, anaamua kusaka mke au mume
mwingine. Unapoona hali hii imeanza jalibu kuwajilazimisha kuwa karibu yake
sana. Na pale unavyoona hali ni mbaya zaidi basi mweleze rafiki yake wa karibu
ambaye humwamini kwa kila jambo.
Au
unaweza kumweleza mtu anayeheshimika ili asikilize kilio chako na mwisho wa
siku utaona mafanikio. Hii ni kwa wachumba na hata kwa wanandoa itapotakiwa
kufanya hili.
Kwa
wanandoa ni muhimu wawaone pia wezee wa busara ambao wanaaminika na kukubalika
na jamii. Ikishindikana basi waende katika ofisi ya kata au ustawi wa jamii kwa
msaada zaidi.
2. USO HUONYESHA KUWA HAPENDI
KUONGEA
Ni
hali ya kawaida kuona mke au mme kuonyesha kuwa apendi kuongea na wewe. Sababu
kubwa anayo moyoni na hataki kuisema. Uso mara nyingi unakuwa na asili ya
mkunjo kwa wanawake. Na kwa wanaume sura inakuwa na asili na makunyanzi. Hapo
ujue kuwa hali ni mbaya sana. Hapo hata ukimsesha anaona kama unajisumbua tuu.
Na kama ataamua kusema ni kidogo tu na mwisho inaedelea kukaa kimwa.
Pia
hata majibu yake uteyaelewa tu. Ni ya unyonge hivi, na sauti ya chini isiyo na
mvuto au ushawishi kwa mwenzake. Pakifikia mahali kama hapa jalibu kumnunulia
zawadi mzuri, kumkisi, kumwambia oooo mpenzi wangu….nakupenda sana…….leo
umependeza namna hii….. Kweli mimi nimechagua mke mzuri au mme mzuri sana……kwani
najivunia sana kukuona na kuwa na wewe muda wote.
Wakati
mwingine unaweza kwenda kumsaidia kupika, kuosha vyombo na hata kumwambia
mkaoge pamoja. Utaona jinsi anavyoanza kubadilika mpenzi wako. Hapa hakuna
mchawi bali ni namna tabia yako ulivyomwonyesha. Hali hii haiwezi kwisha ghafla
kama kimbunga bali huenda taratibu na mwisho wa siki hali inajirudia. Kwa hali
ya kawaida uchukua kuanzia siku 21-22. Uendelea kumwambia maneno yenye baraka
na busara bila ya kukata tama. Uwe na imanii ya hali ya juu kwani majibu
utayokutana nayo si ya kawaida, lakini mwisho wa siku hali itarudi kuwa ya
kawaida kabisa.
3. HASIRA ZA
MARA KWA MARA.
Hatua
hii mpenzi wako huanza kuchukia kila jambo. Utende mema yeye kwake ni baya.
Utajiongelesha ni kama unamuongezea hasira. Hapa ndipo watu huwa wanafikia
kuchukua hatua ya kujiua wenyewe kisa mpenzi wake amamsaliti. Mfano wa majibu
utayokutana nayo ni kama haya:-
1. mbona hivi mpenzi?
2. mimi nifanyaje?
Wewe yanakuhusu nini?
Umepata hasara gani mimi kufanya
hivi?
Fanya utakavyo?
Mimi ndo kila kitu?
1. kwa nini yamefikia hapo?
2. we ujui?
Hizi
ni baadhi ya changamoto utazokutana nazo wakati wa maojiano yako na mpenzi
wako. Usimpige kisa majibu ya mkato. Kama mwanaume hali ikizidi kuwa ni kelele
tu, basi kaa kimya au ondoka na kwenda kufanya shughuli zingine. Utavyorudi
atashindwa anzie wapi.
Kama
ni upande wa mwanamke yanamtokea haya basi fanya hivi:- kaa kimya kwa muda,
atakaa kimya mpenzi wako. Kasha usisite kumwandalia mmeo chakula cha kutosha na
kizuri. Hata kama hali usichoke kuandaa. Mpe maneno matamu mkiwa kitandani na kujaribu
kumgusagusa sehemu mbalimbali za mwili. Hapa mwanaume ujanja unaisha hapo.
Kama
hizo njia zinachukuwa muda mrefu basi anza kwa kumuomba msamaha. Hata kumpigia
magoti usione aibu. Piga huku ukionyeshwa kuwa hali hile upendezwi nayo. Ni ya
bahati mbaya. Hakirudi katika hali ya kawaida na siku nyingi kupita anza
kushusha makombola kwa njia ya utani kuwa pale mme wangu kosa lilikuwa lako.
Kama muelewa ataweza kijirekebisha ipasavyo na mwisho wa siku mukarudi kama
siku ya kwanza kuanza penzi lenu.
4. MANENO YASIYOFAA HUANZA
KUZUNGUMZWA
Hii
ni hatua ya nne ambayo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Mpenzi wako
hutamuona mchungu kupita kiasi. Hutaona kama kuna watu wanamfundisha kuongea
maneno haya. Ukweli ni kwamba ukishaona mke wako mara nyingi yeye na wenzake,
hana muda wa kukaa akuandalie chakula (kwa mwanamke aliye kwenye ndoa) basi
ujue kwamba rafiki zake wamemfundisha na ujue kuna jambo linaendelea ambolo
mwisho wake ni kutengana.
Kwa
mchumba basi utaona maneno ya ovyo ovyo ili mradi umwambie sasa mimi na wewe
basi. Atafanya kila aina awezavyo utengane. Hii huweza kuwa mwanaumme ndio kisa
au mke mwenyewe ndio kisa. Akishindwa hapa anaamua kuchukuwa maamuzi magumu
sana ambayo hutasahau tena maishani. Kama vile kumpigia mpenzi wake mpya na
kuanza kuongea naye.
Hiyo
atakuwa amekuheshimu, anamkumbatia na kumkiss ili mradi uhuzunike kwa hili
kasha mtenge ili awe huru. Hali hii huwa ni mbaya zaidi kama mtu umependa.
Hhiki ni sawa na wanavyofanya wanaume walio wengi katika uchumba na doa.
Ukimuuliza namba hii uliyosevu Juma mbona inaonyesha ni hile ya Asha atakuambia
ni rafiki yangu.
Ukiendelea
kumbana atakuambia ni ya mke wangu. Sasa wewe unasemaje au unataka nini? Haya
utokea kwa wote wenye ndoa zao na wale walio kwenye uchumba bila kujali mme au
mke au mchumba.Haya ndiyo yanayojili sehemu hii iwapo utashindwa kutatua hizo
hatua tatu za mwanzo.
Namna
ya kutatua sehemu hii ni kutumia zile njia elekezi ya hatua ya kwanza. Kubwa
zaidi hapa ni kuomba msamaha kwa kile kinachovumilika, na kile ambacho akivumiliki
ni kwenda kwa washauri nasaha kama vile maafisa ustawi wa jamii kwa manufaa ya
wote. Wao watakusaidia vizuri hata kama uko peke yako na mwenza wako alikataa
kwenda huko. Utamsahau na kuiona dunia ni tamu zaidi y asana na utasema
mwenyewe ulichelewa wapi kipindi yanatokea haya.
5. KUDAI KUTENGANA
Kama
mnavyojua, mti uota, ukua, utengeneza majani, huishi na hatimae mwisho kufa.
Hapa mpenzi wako utaona ni balaa tupu. Yaani hafai hata kidogo. Kama una imani
ndogo utatamani uondoke uende mbali ambako hutamwona tena. Hapa hakuna jinsi,
hata mahakama huamua kutenganisha ndoa kama walioana. Hapa usipofanya kama
atakavyo mpenzi wako unaweza kuishia hata gerezani au kuchukua uamuzi wa
kumpiga.
Kweli
inauma sana kumwona mke/mme au mchumba unaempendaanataka mutengane. Wengine
huamua kujinyonga, wengine kunywa sumu, wengine wanaamia baa na kuweka makazi
yao. Mmoja hakikataa hakuna jinsi, mwache aende kwa usalama.
Jinsi
ya kutatua hili ni kwamba unapaswa kwenda kukubali tatizo lililotokea. Kwani
kinachotokea kwa wenzako hata wewe ipo siku yatatokea. Katika maisha ya
binadamu kuna kupenda na kutendwa, hivyo kutengana ni moja ya sehemu ya maisha.
Jaribu kutembelea sehemu zenye mkusanyiko wa watu. Lakini usinywe pombe, na
kama ulikuwa unakunya unaweza kuacha kabisa hatakwa miezi kadha na usitembelee
sehemu za pombe.
Unaweza
kwenda disco na sehemu nyinginezo mzuri kama vile kwenye mpira, kucheza puru,
drafti, bao na hata karata. Hali yako itarudi kama zamani. Utajiona wa kawaida
(hii ni kama kwa mwanaume). Ukikutana naye usimwone kama ni adui ako mkubwa,
kwani yaliyotokea ni majaribu ya dunia. Na pale mkaapo kwa muda mrefu na kuona
kuna umuhimu wa kurudiana basi murudiane kwa moya mmoja.
Kwa
wanawake huchukua muda mrefu kama tendo lilifanywa na mwanaume. Na tatizo
lenyewe kama kumfumania mme au mchumba wake wakiwa katika chumba kile kile
anacholala yeye. Huwa anaona ni unyama. Kwa hili, mke huyu kurudiana naye
itachukua muda mwingi kwani lile swala humrudia mara kwa mara. Na kama
alimpenda sana bwana wake huamua usikuone kamwe.
Lakini
hakuna jambo lisilo na mwisho. Mme unapaswa kwenda kuomba msamaha kwa yule mke
wako uliyemwacha. Kukataliwa kwa mara ya kwanza ni jambo la kawaida, kwani ile
icha itaendelea kumrudia. Jifanye kama usikii, fanya hivi zaidi ya mara tano
hadi kumi. Mke wako au mme wako ataanza kukuonea huruma na hatimae kuwa naye
pamoja.
NB:
ieleweke kwamba si kila unayemfanyia tukio baya ataweza kukusamehe. Ni wachache
wenye nyoyo kama hizo. Bora ubadilike na kutunza utu na uthamani wako mapema.
Kwa kufanya hili maisha utayaona kama maji ya kunywa.
NANI HUANZA KUMWACHA MWENZAKE KATI
YA MKE AU MME
Kuhusu
nani anayepaswa kumwacha mwezake lipo katika sehemu mbili ambazo ni:-
A/ kwa wanandoa
Katika
zama hizi za utandawazi anayepaswa kumwacha mwenzake ni yeyote kati ya mke au
mme chini ya ushahidi na usimamizi wa mahakama. Kila mmoja anayo haki hiyo.
Kinachofanyika ni kwamba mhusika apitie hatua zote za kuachana au kuvunja ndoa
yao.
B/ kwa wachumba
Hapa
ndipo inapoanzia balaa. Kila mmoja anataka aanze mwenzake ili apate ya kusema.
Mwanamke anafanya vituko ili mchumba wake aseme basi kuanzia leo mimi si
mchumba wako. Na mwanaume naye husubili kutoka kwa kwanamke aseme mimi basi.
Hapa ni usanii mtupu kwa sababu hakuna anayezifahamu ndoa hizi zaidi ya
marafiki. Na ikifikiwa kujua wazazi basi ujue muda umekwenda sana.
Nilichogundua
ni kwamba, hawa wachumba utengana tu pale anapopata mchumba mwingine
anayeridhika naye. Kuna baadhi wanakuwa na wachumba kwa ajili ya kupeleka siku
ili ziende. Na mwingine anakuwa amejitoa mhanga katika hili. Kwa mchumba
asiyehitaji kuwa na wewe dalili ni zile zile na ndio hatua zenyewe za kuvunjika
kwa uhusiano.
Hapa
kuna ndoa za siku moja yaani usiku wanapatana asubihi kila mtu kivyake. Mtu
huyu mbinu anayoingia nayo ni ya kumwonea huruma sana, lakini saa chache tu
baadaye hali ni mbaya. Kila ukimgusa mchungu kama pilipili.
Kuna
ule uchumba wa muda mrefu. Ambao watu hukaa zaidi ya miezi mitatu. Hapa
wapendanao huachana kwa ugomvi au kupata kwa mke au mme mwingine ambaye
anaonekana anamfaa.
HALI BAADA YA KUTENGANA
Kwa
walio wengi hapa hali hubadilika na kuwa tofauti na mwanzo. Lakini ukweli ni
kwamba hutokea hali za aina kuu mbili ambazo ni hali ya maelewano na hali ya
kutoelewana.
A/
Hali ya kutoelewana
Hapa
kama wapenzi hawakubahatika kuwa na mtoto basi kila mtu huanza kumchukia
mwenzake na kufikia hatua ile hata kuto salimiana. Ieleweke kuwa hii ni kwa
baadhi ya watu tu. Na kama mlikuwa na watoto basi mawasiliano hukata kwa muda
mfupi na baada ya kupita siku kadhaa huanza kuwasiliana kama mwanzo ijapokuwa
kila mmoja hapendi iwe hivyo. Hii hutokea kwa sababu kila binadamu ana kichaa.
Na kichaa uweza kuondoka na hali ikarudi kama ya zamani.
Kipindi
hiki mwenza wako yupotayari hata kukuondoa duniani, na kwa kuwa sheria humbana,
hutamani kwenda mbali sana ili mradi asikuone au msionane. Maisha huendelea, na
kama hatatokea mtu ambaye anaweza kumweka sawa (counceling) busi hutokea ile
hali ya chuki juu ya jinsia fulani.
Kama
alikuwa ni wa ofisini basi utaona mambo yanageuka na kuanza kuwa mkali kwa ile
jinsia tofauti. Hapa kama ni mwajili mkuu basi anauwezo hata wa kukukaripia
kama motto au kukufukuza kazi kabisa ndani ya masaa 24.
Ushauri
wangu ni kwamba, ukiona hali hii imeanz kutokea kwa mfanyakazi mwenzako au
mwajiliwa mwenzako, au yule mpenzi uliyemwacha na hata ndugu yako, naomba uwe
naye karibu sana hata kama maneno unayopewa ni ya kukatisha tama. Endelea
kumsaidia kazi ndogo ndogo, kufanya mazoezi ya viongo, kutembelea maeneo
mbaalimbali na kumshauri mutembelee zile ofisi za ushauri nasaha kwa ajili ya
kuweza kumrudisha hali yake kuwa ya kawaida.
Inachukuwa
muda mrefu sana kukubaliana na wewe kuwa mpenzi wako aua rafiki yako mpendwa au
hata ndugu yako kukuelewa kuwa ana tatizo. Hapa hujikuta kila jambo analofanya
na kuamua liko sahihi. Usikate tama juu ya majibu unayopewa. Yatumie majibu
hayo kama changamoto kwako. Mtu ambaye huweza kumsikiliza mtu wa namna hii ni
yule tu aliye karibu naye tu.
Hali
hiyo huweza kutoweka mapema kutegemea na wale walionae karibu wanavyomshauri
mlengwa. Ikumbukwe kwamba si kila rafiki ana maneno ya busara kwako. Huyo
rafiki yako ndiye mbaya wako wa kesho. Leo anakupenda na kesho anakugeuka. Na
si kila rafiki ni mbaya kwako. Unatakiwa kuangalia rafiki yupi ni bora zaidi na
anayekufaa ili akusaidie wakati wa shida badala ya kukuangamiza.
B/
Hali ya maelewano
Hapa
wapendanao huendelea kuwasiliana vizuri kama kipindi cha penzi lao. Hali
inakuwa tofauti kidogo lakini mawasiliano ni mazuri. Hii hutokea pale mke au
mme au mchumba wameachana kwa njia ya amani.
ATHARI ZA KUPENDA KUPITA KIASI
Ni
vyema kujua mpenzi wako anakupenda kiasi gani. Na kila mtu ni siri yake
mwenyewe kujua anampenda mwenzi wake kwa kiasi gani. Kumpenda mke au mme au
mchumba wako ni jambo jema sana. Muonyesheshe namna upendavyo kwa maneno,
pamoja na tabia yako.
Kuna
jambo moja ambalo mtu yeyote apendezwi nalo kuona mme, mke au mchumba
akilitenda ambalo ni kuonyesha dharau ikiwemo kuona maneno anayozungumza hayana
mantiki yeyote. Akigundua mwezi wako ujue kuwa hali ya penzi lenu linaelekea kubaya. Si vizuri kuendekeza hali
hii kama umezaliwa nayo au kurithi kutoka kwa wazazi. Inapaswa ujizuie.
Hakuna
mapenzi ya kweli kama hakuna upendo. Katika maisha ya sasa ni muhimu sana
kuonyesha namna unavyompenda mke/mme wako. Watu hupenda sana kiasi kwamba hata
kufikiri suala lingine, badala yake huitaji kukaa muda wote na kumfuata kila
aendako. Na wengine ufikia mahali hadi anaharibu kazi. Kila kazi anafanya ili
mradi aonekane amefanya kazi.
Kwa
kawaida imezoeleka kuona mke au mwanamke ndiyo anayependa sana kuliko mme wake.
Kiukweli ni kwamba wote wana haki ya kuonyesha kila aina ya upendo alionao kwa
mweza wake.
Zifuatazo
ni athari za kupenda kupita kiasi kwa wapenzi:-
-Kushindwa
kutekeleza majukumu ya kila siku ikiwemo ya kiofisi kwa wafanyakazi.
-Siku
ya kutendwa ikiwadia basi kwa aliyetendwa ni rahisi kupata mshtuko wa moyo
(stress) au kujiua.
-Kutosalimiana
kwa muda mrefu.
-Kushindwa
kusaidiana kwa namna moja au nyingine hasa yale yaliyo nje ya mpaka.
Nadhani
umejifunza mengi sana katika kitabu hiki. Ni jukumu lako kubadilika na kuwa
katika mstari mnyoofu. Mpende mke/mme au mchumba wako lakini usipitilize
kiwango kiasi kwamba unapoteza welekeo wa maisha yako. Utaumia na kushindwa
kufanya maamuzi yako kwa wakati husika.
Maoni yenu ni muhimu sana kwangu. Unaweza
kutuma kwa anuani zifuatazo:-.
MAWASILIANO
facebook account- AUSI CHIWAMBO
twitter account- ACHIWAMBO
Arasachi the center of Learning, on
facebook
http://sociologist-baso.blogspot.com
Phone No. 0753 110740
0652 403792
Kazi hii imeandaliwa na
CHIWAMBO, A. R. (2011)
BA SOCIOLOGY
TEOFILO KISANJI UNIVERSITY (TEKU).
No comments:
Post a Comment